Breaking News
recent

IGP SIRO AZUNGUMZIA MIILI ILIYOOKOWA COCO BEACH

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amesema wameunda timu ya wataalamu kuchunguza miili iliyookotwa na sampuli kutoka miili hiyo zimechukuliwa.

Amesema iwapo kuna watu ambao ndugu zao wamepotea ni vyema wakafika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa ajili ya vipimo na kufanyika upelelezi.

“Bahari ni kubwa inapita katika nchi nyingi na inachukua kila kitu, haya mambo yanapotokea hata nchi nyingine yanatokea, kwa hiyo kimsingi tumeunda timu ya wataalamu ya kupeleleza kuhusu miili hii, wamechukua majimaji kutoka mwilini,” alisema IGP Sirro alisema,

 “Kama kuna mtu ambaye ndugu yake amepotea afike makao makuu ya Polisi upande wa DCI tuweze kufanya uchunguzi kuona kama ni ndugu yake.”

Alisema miili hiyo haijabainika kuwa ni ya watu wa Taifa gani. "Tatizo letu Watanzania ni kwamba moja kwa moja wanahanza kuhisi kwa nini tunakuwa tunaishi kwa kuhisi na hii hisia si nzuri tuseme kitu tukiwa na huhakika ikitokea jambo utasema ni Sirro utasema ni nani, hii si nzuri na niwaambie tumwogope Mungu pia"alisema Sirro

Na Brighiter Masaki


No comments:

Powered by Blogger.