Breaking News
recent

KICHUYA NI HABARI NYINGINE


Mchezaji wa timu ya simba shiza ramadhani kichuya ameonesha makali yake jana katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara kati ya simba dhidi ya stand united  uliochezwa katika uwanja wa kambarage mjini shinyanga katika mchezo huo kichuya alionesha kiwango cha juu na kuweza kuipatia bao safi la kuongoza bao ambalo alifunga kwa ustadi mkubwa baada ya kupokea pasi toka kwa john book Adebayo bao ambalo lilidumu adi mwishoni mwa kipindi cha kwanza



Aidha kipindi cha pili mchezaji huyo alionesha uwezo Zaidi kwa kushirikiana na wenzake na kuifanikishia timu yao kupata bao la pili kupitia kwa  mavugo aliyeingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya mganda Emanuel okwi aliyetoka mwanzoni mwa kipindi cha pili

Hata hivyo timu ya stand pia ilifanikiwa kupata bao moja kupitia mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa simba kushika eneo la penati na refa kuamuru penati na adi kufika mwisho mchezo ulimalizika kwa timu ya simba kuibuka na ushindi wa bao mbili kwa moja na kuiwezesha timu hiyo kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara kwa kuwa na alama 11 ikifuatiwa na mtibwa sugar ambayo nayo ikiwa na alama 11 ikitofautiana idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Na Hamad Nasibu

No comments:

Powered by Blogger.