RAMMY KUIGIZA NA AKI NA UKWA.
Msanii wa Filamu za Bongo Rammy Galis, ameweka wazi kisa
cha Filamu anayokwenda kushiriki nchini Nigeria Mwisho wa mwaka huu na
Wachekeshaji wakongwe Aki na Ukwa.
Akizungumza Rammy alisema kuwa, ataigiza kama Shemeji wa
Wachekeshaji hao wawili ambaye hana Mkwanja na amesafiri mpaka Nigeria
kwenda 'Kumchuna' Dada yao.
"Story iko hivi Aki na Ukwa ni mashemeji zangu lakini sina
kitu Ila Nina mapenzi ya kweli, sasa nimesafiri mpaka Nigeria kwenda
kumfata Dada yao na nimefikia nyumbani kwao, kwa hiyo Aki na Ukwa wananifanyia vita ili nirudi Tanzania kwa kuwa sina kitu, wanamtafutia
Dada yao Wanaume wenye pesa"
" Ila kikwazo ni Mimi kwa kuwa Dada yao ananipenda sana,
kwa hiyo wananifanyia visa vingi Mara maneno Mara nafungiwa nje Dada yao
akienda kazini yaani ni Taflani Mtindo mmoja" alisema Rammy Galis.
Katika hatua nyingine Staa huyo wa Filamu ya Chausiku,
amedai Japokua anafahamu wapo baadhi ya wasanii ambao hawaonyeshi
kufurahishwa harakati hizi lakini itabidi tu wakubali, Rammy ndio
anaweza kuwa ngazi ya kwanza katika kuipeperusha bendera taifa letu
katika tasnia ya filamu.
Na Brighiter Masaki.

No comments: