ASLAY KUUFIKISHA MUZIKI WAKE KIMAAIFA.
Msanii wa Bongo Fleva Aslay amesema
anataka kuupeleka mziki wake kimataifa,Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya
vizuri na ngoma yake mpya ‘Natamba’
Akizungumza Aslay alisema kuwa
anaona muziki wake kwa upande wa nyumbani umeshakubalika hivyo mipango yake siku
za mbeleni kufanya hivyo.
“Nataka nivuke kimataifa, unajua
siwezi kufanya muziki tu nipo nyumbani, kwanza naogopa kuzoeleka na watu nataka
nivuke kimataifa baadae niwe na maisha yangu ambayo naweza kusema namsaidia mtu
akatoboa sehemu fulani,” alisema Aslay.
Aliongeza kuwa anaamini kutoboa
kimataifa kutamuimarisha kisanii na kiuchumi hivyo ataweza kuwasaidia vijana
wengine wenye viapaji kupitia label yake ambayo ipo tayari kwa sasa.
Na Deogratius David.

No comments: