Breaking News
recent

CALISAH NITAVAA HATA GAUNI NIKIPEWA MILIONI 10.

Mwanamitindo wa Bonngo Calisah,  ambaye hivi karibuni ameshangaza ulimwengu  kwa kupiga picha akiwa amevaa viatu vya kike, amefunguka kuwa yeye ni mfanyabiashara kwa hiyo yuko tayari hata kupiga picha na gauni endapo atalipwa dau pesa shilingi milioni kumi.
Akizungumza Calisah ambaye kwa sasa amegandwa kama ruba midomoni mwa watu kutokana na picha hizo, alisema:


“Siwezi kukataa Mkwanja kwa kuhofia watu wataongea, kitendo cha kuvaa viatu na kupiga navyo picha wala siyo vibaya, ingekuwa nazurura navyo mitaani hapo sawa. Waendelee tu kuongea mimi naingiza mtonyo na siyo viatu tu, mtu yeyote atakayeweza dau  langu la million kumi hata gauni nitavaa.”alisema Calisah

Mwanamitindo huyo alisema kuwa baada ya picha  hizo kusambaa mitandaoni, familia yake ilichukia sana kiasi cha kumweka ‘kitimoto’ kwenye ‘Whatsapp Group’  la familia, kitu ambacho kilimuumiza sana, ila ilifika muda wakamuelewa.

Na Brighiter Masaki.

No comments:

Powered by Blogger.