MR UNIVERSE MATUKIO ATANGAZA FURSA KWA VIJANA
MR Universe Tanzania mwaka 2002,Matukio Chuma,amewataka
vijana wa Kitanzania kutumia fursa mbalimbali
zinazojitokeza ndani na nje
ya nchi kuliko kulalamika kuwa hakuna
fursa.
Akizungumza na waandishi,,katika uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere uliopo jijini Dar es salaam,
baada ya kuwasili akitokea Marekani ambako ndiko anapofanyia shughuli zake za uandishi wa vitabu na
mashairi, ujasiriamali uhamasishaji, Chuma alisema kuwa sasa ni wakati
wa vijana wa Kitanzania kuthubutu
na kutumia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitangazwa
duniani.
“Nawashukuru watu wote waliojiokeza na kwamoyo wa upendo walionionyesha, baadhi ya
marafiki zangu kwa kuja kunipokea, ushauli na kilio change ni kwa vijana
wenzangu wa Kitanzania ni kuthubutu na
kutumia fursa mbali mbali ambazo zimekuwa zikitangazwa duniani kama
ambavyo mimi nilithubutu na ninazidi kuendelea kuthubutu ndio siri kubwa ya
mafanikio yangu”alisema Chuma
Aidha Chuma aliongeza kwa kusema kuwa yeye yupo eyali kwa kijana yeyote wa kitanzania
ambaye ataitaji msaada wa kupata Fursa
yupo ayari kumsaidai bega kwa bega katika kufanikisha ndoto zao.
Na Brighiter Masaki


No comments: