MSIGWA AANIKA MBINU WALIZOTUMIA IRINGA KUWANASA MADIWANI WANAODAIWA KUPOKEA RUSHWA.
Mbunge wa Iringa Mjini kwa
tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kuhusiana na biashara
ya kununua madiwani wa CHADEMA pia ilifanyika Iringa na kusema kuwa wao
walitumia vifaa kutoka Australia kubaini hilo.
Peter Msigwa amesema hayo
leo jijini Dar es Salaam baada ya kutoka Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambapo walikwenda kuwasilisha ushahidi wa Rushwa
dhidi ya kununuliwa kwa madiwani hao na wateule wa Rais John Pombe Magufuli.
“Iringa
mjini biashara nayo ilifanyika na nina ujasiri mkubwa kwamba muhusika mkuu wa
biashara ya kununua madiwani Iringa Mjini ni ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa
Wilaya pamoja na baadhi ya polisi.
“Hiyo
mliona ‘Episode ya Arusha’ vilitumika vifaa vya Uingereza kule Iringa
tulitumia vifaa vya Australia na sisi tutafungua jalada kama ambavyo Mkurugenzi
wa TAKUKURU ametushauri kwa hiyo tusubiri sababu tumekabidhi kwenye korido za
serikali na tunataka sheria zichukue mkondo wake huu uongo uongo wa kusema watu
wanaunga mkono utendaji wa serikali tunataka ufike mwisho ili watu wakae kwenye
nafasi zao kwa haki na jinsi ambavyo watu waliamua kuwachagua,”alisema Msigwa
Na
Brighiter Masaki.

No comments: