BEN POL ATAJA SIFA ZA MWANAMKE ANAEMUITAJI.
Msanii wa muziki wa kizazi
kipya nchini Ben Pol amesema kitu pekee anachokiangalia kwa mwanamke
ambaye ataweza kumpenda na kuwa naye na mahusiano ya kimapenzi ni lazima
awe anajiamini pindi wakiwa wanaongea au hata wakiwa wanachati.
Ben Pol amefunguka hayo baada
ya kupita siku chache, aliyekuwa anadaiwa kutoka naye kimapenzi ambaye ni
msanii wa vichekesho nchini, Anastazia Kisaveli, anayefahamika kwa jina la
‘Ebitoke’ kulalamika kwamba hapokelewi simu zake wala kujibiwa ujumbe mfupi
pindi amtumiapo Ben Pol.
“Endapo nikimpenda msichana sifa kubwa huwa naangalia kujiamini kwake,
pindi tukiwa tunaongea na kuchati, usafi wake, umakini na uharaka katika kujibu
kitu au vitu ambavyo anaulizwa kwa wakati huo,” amesema Ben Pol
Mwanamuziki huyo kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Kidume’ ambao amemshirikisha msanii kutoka Nigeria anayejulikana kwa jina la Chidnma.
Na Brighiter Masaki

No comments: