Breaking News
recent

DOGO JANJA UWOYA NI MSHIKAJI WANGU.

Mkali wa ngoma ya Ngarenaro Abdulaaziz Chende’Dogo Janja’, amefunguka kuwa skendo inayosambaa ikimhusisha yeye na Malkia  wa Bongo Muvi, Irene Uwoya, kuwa wanavunja wanamahusiano ya kimapenzi  kisiri, ishu hiyo imeleta mgogoro kati yake na mpenzi wake, ambaye anadhani huenda labda ishu hiyo ina ukweli wowote  ndani yake.

Dogo janja ambaye hata ashikiwe mtutu wa bunduki, hajawahi kukubali kuwa na mahusiano ya kimapenzi  na Uwoya,  alisema kuwa yeye Uwoya ni mshikaji wake tu wanawasiliana mara chache sana nasi vingine.

“Sina uhusiano wa kimapenzi na Uwoya, kwanza hii ishu imeniletea ugomvi na Mamlai wangu {mpenzi wake}, ni stori ambazo zipo nazisikia, Uwoya ni mshikaji wangu tu tunawasiliana mara chache sana, lakini mapenzi naye sina.”alisema Dogo Janja.

Na Brighiter Masaki.

No comments:

Powered by Blogger.