UN Yaitaka DRC Kutangaza Kalenda Ya Uchaguzi
Umoja wa mataifa umeitolea mwito mkali serikali ya Jamhuri
ya kidemokrasia ya Kongo kuhusiana na kutangaza haraka tarehe ya uchguzi na
kuweka mikakati ya kuhakikisha uchguzi huo unafanyika katika mazingira yenye
utulivu na amani.
Mkutano huo uliofanyika pembezoni mwa mkutano wa baraza kuu
la umoja wa mataifa na ulioitishwa na naibu katibu mkuu wa umoja huo Amina
Mohammed, pia mkutano huo uliobeba ujumbe wa umoja wa ulaya, Uingereza, Umoja
wa Afrika, Jamhuri ya ushirikiano wa kiuchumi ya Kusini mwa Afrika, SADS,
Jamhuri ya nchi za Afrika ya kati na
Kongo yenyewe.
Lengo kuu la mkutano huo lilikuwa ni kuja na mtazamo wa
pamoja na kuhusisha wadau wote kuelekea uchaguzi wa amani na wa kidemokrasia
nchini Kongo.
Na Kheri Yahaya Ramadhani

No comments: