MANARA:OMOGI BADO NI KOCHA WA SIMBA
MANARA:OMOGI BADO NI KOCHA WA SIMBA
Timu ya simba kupitia
kwa msemaji wao Haji Manara imekanusha vikali uvumi uliokuwa ukienea kwenye
mitandao ya kijamii juu ya klabu yao kuachana na kocha wake mkuu Joseph Omogi.
Akizungumza na kituo cha redio Efm katika kipindi cha E
Sport msemaji wa timu hiyo amesema taarifa ya timu hiyo kuachana na kocha wake mkuu sio za kweli
bali ni uvumi tu wa baadhi ya watu ambao
hutumia mitandao ya kijamii kueneza taarifa za uongo, kuichafua klabu hiyo na
kwamba klabu hiyo hai ana mpango
wakuachana na kocha wao huyo”alisema
Aidha msemaji wa timu hiyo ameiomba mamlalaka ya mawasiliano
kuwachukulia hatua watu ambao wana tabia za kueneza taarifa za uongo kwenye
mitandeao ya kijamii ili iwe fundisho kwani taarifa hizo husababisha taaruki na
usumbufu kwa watu
katika hatua nyingine timu hiyo inatarajia kushuka
dimbani mwishoni mwa juma hili siku ya
jumapili kucheza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya stand united ya mkoani shinyanga katika uwanja wa
kambarage ikumbukwe kwamba katika mchezo huo timu ya simba inaitaji ushindi wa
aina yeyote ili ijiweke nafasi nzuri katika msimamo wa ligi kuu hasa baada ya
timu hiyo kutoka sare katika mchezo uliopita
Na Hamadi hamadi

No comments: