Breaking News
recent

HAMISA NIMEKUBALI KUWA MKE MDOGO.

Mwanamitindo na Video Qeen Bongo,  Hamisa Mobeto ameweka wazi  uhusiano wake na mjasiriamali Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuwa yupo tayari kuwa nyumba ndogo, hana tatizo na mke mwenzake huyo na hamchukii kwa sababu watoto wao ni ndugu.


Alisema awali hakuwa anamkubali mke mwenziye huyo lakini kwa sasa hana budi kumkubali hana chuki kwa kuwa wote ni wake wa mtu mmoja kwa hiyo hawapaswi kuwa na matatizo yeye hana tatizo nae.
“Mimi sina tatizo naye kwa sababu watoto wake ni watoto wangu kwa hiyo mimi sina tatizo ipo siku watoto wale (wa Zari) watataka kuja kumuona ndugu yao au huyu wangu atataka kuwaona ndugu zake, tutawaruhusu tu kwa sababu sisi wote ni wake wa mtu mmoja, kwa hiyo hatupaswi kuwa na matatizo, mimi sina tatizo naye,” alisema Hamisa Mobeto

Kuhusu madai ya kupewa shilingi 70,000 kila siku yaliyosemwa na mzazi mwenzake hivi karibuni, Mobeto alifafanua kwa kusema kuwa kama mtu mzima lazima hujue motto anahitaji nini na nini na mbaka anaenda mahakamani nyuma yake kuna watu wanamsimamia.

“Kama mtu mzima lazima ujue kuwa mwanamke mwenye mtoto anahitaji nini na nini, unapokuwa na mpenzi wako au mke wako huwezi kushindwa kumpa hiyo elfu sabini au laki moja, kwanza mimi na yeye tulikubaliana kuzaa siyo kama mimi nilimlazimisha hapana, halafu mpaka mimi nakwenda mahakamani ni kwa sababu nyuma yangu kulikuwa na watu wananisimamia ndiyo maana nikapeleka hili suala mahakamani ili malezi ya mtoto yaje, basi yeye alimleta mwanasheria wake wakakutana na mwanasheria wangu hivyo hayo mambo tuyaache kwanza”aliongeza Hamisa


Na Brighiter Masaki

No comments:

Powered by Blogger.