NASSARI; NIPO KWENYE BONDE LA UVULI WA MAUTI
MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki
(CHADEMA) Joshua Nassari amefunguka na kusema maisha yake yapo hatarini na
kudai kuwa watu ambao amewaanika kwenye sakata la ununuzi wa madiwani
wanamtafuta.
Nassari amesema hayo ikiwa imepita
siku moja toka alipokwenda kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) kupeleka ushahidi wake juu ya madiwani wa CHADEMA waliohama
chama kwa kuhongwa rushwa na wateule wa Rais John Pombe Magufuli.
“Maisha yangu yapo kwenye bonde la
uvuli wa mauti, Maisha yangu yapo hatarini kwani Watesi wetu wananitafuta”
aliandika Nassari kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Mbali na hilo wachangiaji mbalimbali
kwenye ukurasa wa Mbunge huyo walimtaka azidi kumuomba Mungu huku wakimshauri
kuongeza ulinzi zaidi katika maisha yake ya kila siku kutokana na jambo ambalo
ameliibua na kumtaka aendelee kupambana, baadhi ya wachangiaji wengine wamedai
kuwa anachofanya ni njia ya kujitafutia umaarufu kisiasa.
Juzi Mbunge Joshua Nassari,
Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa
walikwenda kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na
kupeleka ushahidi wao juu ya sakata la kununuliwa kwa madiwani wa CHADEMA na
kuhongwa fedha na ahadi mbalimbali kutoka kwa wateule wa Rais mkoani Arusha.
Na Brighiter Masaki.

No comments: