OCTOBER 6 YA MANJI
Hukumu ya kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili
mfanyabiashara Yusuf Manji itasomwa October 6 mwaka huu baada ya
mahakama ya Kisutu kupitia Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian
Mkeha kufunga kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi.
Manji akiwa na mahakamani hapo na wakili wake.
Waliotoa
utetezi wao leo ni pamoja na sekretari wa Manji, Maria Rugarabamu ,
daktari Mkuu wa Zahanati ya Gereza la Keko, Inspector Eliud Mwakawanga,
pamoja na Daktari Bingwa wa Afya ya akili na dawa za kulevya, Francis
Benedict kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke ambapo kila mmoja aliieleza
mahakama kile anachokijua kuhusu tuhuma za mfanyabiashara huyo kutumia
dawa za kulevya.
Mahakama ilipokea risiti za dawa
ambazo alikuwa anaandikiwa Yusuf Manji na ofisi ya Mganga Mkuu wa
Zahanati Magereza ya Keko, Inspector Eliud Mwakawanga kama vielelezo kwa
upande wa utetezi.
Mganga huyo amesema Manji alikuwa anatumia vidonge 30 kila siku ili kuimarisha afya yake.
Alisema
kuna wakati ambao Manji alikuwa anaamka akiwa kama amechanyikiwa lakini
akimpatia dawa anarudi katika hali yake ya kawaida, kwa
upande wa shahidi wa tatu ambaye ni Daktari Bingwa wa Afya ya Akili na
Dawa za Kulevya kutoka hospitali ya Rufaa ya Temeke, alisema kuna baadhi
ya madawa ya hospitali akitumia mgonjwa mkojo wake ukipimwa utakutwa na
chembe chembe za Morphiem ambazo pia hupatikana katika mkojo ya watu
wanaotumia dawa za kulevya.
By Douglass David

No comments: