DIMPOZ AACHIA CHECHE
Angalau kwa sasa Ommy Dimpoz anaweza akapumzika baada ya
kuutua mzigo mzito wa lawama kutoka kwa mashabiki wake kuhusu kuchelewa
kutoka kwa video ya wimbo wake mpya ‘Cheche’.
Hata
hivyo hali hiyo inaweza ikawa ni neema kwa msanii huyo kutokana na
mashabiki kutamani kuiona kwa muda mrefu. Video hiyo imefanikiwa kushika
namba moja kwenye trending ya mtandao wa YouTube na kuzipiga chini
video nyingine zilizouteka mtandao huo ikiwemo ‘Seduce Me’ ya Alikiba,
‘Zilipendwa’ ya WCB na ‘Unaibiwa’ ya Rayvanny.
Wakati huo huo, Cheche imefanikiwa kutazamwa mara 121,998 katika siku moja tangu ilipowekwa kwenye mtandao huo.
By Ester Mboga
By Ester Mboga

No comments: