ASLAY NILIANZA PEKE YANGU NTAMALIZA PEKEANGU
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva nchini Aslay Isihaka anayeongoza kwa
kupachikwa majina mbalimbali na kufananishwa na wasanii wakubwa kimataifa,
amesema kuwa baada ya kundi la
Yamoto Band
kuvunjika, yeye anaendelea vizuri na kazi zake wala hamna anachokikosa kwa
sababu wakati anaanza hakuwa na kundi.
Aslay aliliambia Ebridensa kuwa alianza muziki akiwa peke yake
na alikuwa na umri mdogo hivyo hata sasa ninauwezo wa kuendelea pasipo kuwa na kundi. Aslay
ambaye kwa sasa anatamba na ngoma zisizohesabika kama vile, likizo, Baby Pusha,
Nyakunyaku, Mhudumu na nyingine nyingi, alisema kuwa:
“Nilianza muziki nikiwa peke yangu na nilikuwa mdogo
kiumri, enzi zile za ‘Naenda kusema kwa mama’, ila niliweza kufanya
vizuri, kwa hiyo kuingia kwenye kundi na kutoka sioni kama nitashindwa
kuendeleza muziki wangu. “Kwa sababu naona ni kama zamani tu, ndiyo maana
nafanya vizuri, naachia Ngoma kila kukicha, na ngoma zangu kali na
zinapendwa, mashabiki hawawezi kuzichoka kwa sababu mimi ni mwanamuziki mzuri,
najua nini ninachokifanya, na sitegemei kushuka kimuziki”alisema Aslay
Aslay ni mmoja kati ya wanamuziki waliokuwa wakiunda kundi la
Yamoto Band, kundi ambalo lilifanya vizuri sana ndani na nje ya nchini kupitia
nyimbo zao kali kama Nitakupwelepweta,Cheza kwa madoido, Niseme Nisisema na
Su waliyomshirikisha mwanadada Rubi.
Wasanii wengine waliyokuwa wakiunda kundi
hilo ni Eneck Bela’The Base Maromboso na Beka Flavour.
Na BRIGHITER MASAKI

No comments: