MBASHA AKANA KUTELEKEZA WATOTO
MWIMBAJI wa Injili Tanzania, Emmanuel Mbasha, ameamua
kuvunja ukimya juu ya tuhuma alizopewa za kutelekeza watoto aliozaa na wanawake
tofauti na kusema habari hazina ukweli wowote ule.
Akihojiwa na kituo kimoja cha radio jijini Dar es Salaam,Emmanuel
Mbasha amesema
tuhuma hizo ni uongo na anachukia watu wanaotengezea habari hizo, kwani yeye
hahitaji habari za kutunga ili kupata kiki kwa kuwa yeye si mwanamuziki wa
Bongo Fleva.
“Si kweli, hivyo vitu ni vya uongo tena nakanusha kabisa. Hivi
kwa nini vitu vingi vinaongelewa vya uongo? Sipendi uongo, hivyo ni vitu vya
Bongo Fleva bhana, mimi sipo kwenye kutafuta kiki wala kuongelea vitu ambavyo
havina faida,” alisema Emmanuel Mbasha.
Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba Emmanuel Mbasha
amewazalisha wanawake wawili tofauti na kuwatelekeza, kisha kukimbilia kwa
mwanamke mmoja mwenye uwezo kipesa hapa mjini Dar es Salaam na kuweka kambi
hapo na huyo mwanamke mpya.
Na BRIGHITER MASAKI

No comments: