LULU AWAHASA VIJANA KUJIAJIRI.
Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameweka wazi kuwa
huu sio wakati wa kutoa wito kwa vijana bali ni wakati wa kufanya kazi kwa
bidii.
Akizungumza lulu alisema kuwa amechoshwa na kutoa wito kwa vijana wanaojibweteka
majumbani kila siku kuwaambia wajishugulishe.
“Huu sio wakati wa kupeana au kutoa wito kwa vijana
wasiojishugulisha na jambo lolote kama mtu anashindwa hata kutumia kipaji chake
alichopewa na Mungu huyo tena basi , ni wakati wa kufanya kazi kwa bidii kwa
watu wote ilikujipatia kipato kilicho halali.alisema Lulu
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa nimejifunza kitu kuwa na biashara
kubwa sio kuwa na pesa nyingi kidogo ulicho nacho ndicho kitakacho kusaidia
wewe kufanya mambo makubwa mfano Ally Rehmtulah alisema kuwa yeye alianza
biashara yake ya mitindo kwa kiasi cha pesa sh elfu 40.
Na Brighiter Masaki.

No comments: