MOTO WATEKETEZA MAKAZI YA WATU 11 TABATA SEGEREA
Moto mkubwa
uliosababishwa na shoti ya umeme umeunguza nyumba moja mali ya Bw. Hamis Rajabu
pamoja na kuteketeza thamani zote na kuziacha familia hizo kutokuwa na mahali
pakwenda.
Familia hizo zilikumbwa na kadhia hiyo siku ya Jumatatu wiki hii maeneo ya Tabata Segerea, ambapo kikosi cha zimamoto kilifika eneo hilo kwa jitihada za kutaka kuuzima pasipo mafanikio.”Sijui ni seme nini ilikuwa ni majila ya saa tisa alfajiri ghafla nikasikia kelele za wapangaji nikatoka nje kutaka kushuhudia lakini ulikuwa moto mkubwa ukitoka katika soketi bleak” Alisema Hamis.
“Siwezi
zungumzia kwa sasa nikiasi gani cha gharama zilizowezakuteketea katika ajali
hii kwani nimapema mno kuelezea tukio hilo”. Alisema Hamis
Baadhi ya
mashuhuda wa ajari hiyo Hamza Ramadhani alisema “moto ulianza kwenye soketi
bleka na kuanza kusambaa nyumba nzima tulijitahidi kadri ya uwezo wetu kuweza
kuokoa baadhi ya mali lakini moto ulituzidi nguvu,Hata hivyo
dereva wa gari la zimamoto alielezea baadhi ya changamoto zilizopelekea
kushindwa kufanikisha kuuzima moto huo ni pamoja na miundo mbinu ya maeneo hayo
kuwa mabovu kwani nyumba hazipo katika mpangilio wa kuruhusu magari makubwa
kuweza kupita kwa urahisi zaidi.
By Hance Mwaisemba
By Hance Mwaisemba

No comments: